Urusi yatoa onyo kali nchi za Ulaya
Urusi imeyaonya mataifa ya Ulaya, kwamba italishambulia taifa lolote litakalothubutu kuchukua mali yake baada ya ripoti kuwa EU inapendekeza kutumia mali ya mabilioni ya dola ya Urusi iliyozuiwa ili kuisaidia Ukraine.