China yapinga kuongezeka operesheni za Israel Gaza
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China, Lin Jian amesema China inapinga vikali ongezeko la operesheni za kijeshi za Israel huko Gaza na kulaani vitendo vyote vinavyodhuru raia na kukiuka sheria za kimataifa baada ya Israel kufanya shambulio kubwa la ardhini katika mji wa Gaza.