Tuesday , 26th May , 2015

Msanii wa muziki Mwasiti Almasi ameeleza kuwa, licha ya kuipenda tasnia ya filamu, kukubali kwake kufanya movie ni mpaka awekewe dau kubwa sana, ama filamu atakayoshiriki iwe na utofauti mkubwa, na pengine kugusia elimu na mambo yanayofanana na hayo.

Mwasiti

Mwasiti ameeleza kuwa, amewahi kufikiria suala hilo, na kwa mtazamo wake baada ya miaka 30 au zaidi mbele ndiyo atakuwa tayari kufanya filamu rasmi.

Msani huyo amekazia kuwa, suala hilo ameliweka pembeni kwa sasa, huku mazingira na uwezekano wa mashabiki wake kumuona katika filamu yakiwa madogo, kutokana na kauli yake kuwa inategemeana na muongozo wa filamu husika.