Wednesday , 29th Apr , 2015

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali PAC, imekataa kupitisha bajeti ya hesabu za mkoa wa Rukwa kutokana na baadhi ya malipo yaliyofanywa kutokuwa na nyaraka huku magari kumi yaliyotolewa kwa ajili ya maendeleo kubaini yaliuzwa kiutata.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali PAC, Bi. Amina Mwidau.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Amina Mwidau amesema hayo jana kwenye kikao cha kamati hiyo ambacho sektretarieti ya mkoa wa Rukwa iliitwa kuhojiwa kuhusiana na bajeti ya mkoa huo mwaka 2012/2015.

Mh. Mwidau amesema mapungufu yaliyopo katika ripoti ya hesabu za mkoa wa Rukwa ni malipo yenye shaka ya zaidi ya zaidi ya shilingi milioni 20.6 ya uchapishaji wa vitabu kwa ajili ya maadhimisho ya mika 50 ya uhuru.

Aidha amesema mapungufu mengine ni matengenezo ya magari yaliyogharimu milioni 44 na viongozi wa sekretarieti ya mkoa kuuziana magari yaliyotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika mkoa huo..