Akizungumza na East Africa Radio, Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui amesema, anaamini watoto hao kutoka shule mbalimbali jijini Dar es salaam watakapomaliza mafunzo hayo watakuwa wamepata somo kubwa sana kwa upande wa michezo litakaloweza kuwasaidia hata watakapo rudi katika masomo ya darasani.
Nyambui amesema, watoto hao ambao wanashiriki mazoezi ya michezo mbalimbali kama riadha na mpira wa miguu wataweza pia kujiajiri kupitia kimichezo pale watakapokuwa wamemaliza shule.