Monday , 27th Oct , 2025

Jumla ya vituo 384 vya kupigia kura vimeandaliwa katika Jimbo la Mwibara na Bunda katika kata kumi na tisa ili kurahisisha zoezi la upigaji kura ambapo kila kituo kimoja kitahudumia wananchi wasiozidi 450.

‎Hayo yamebainishwa na Msimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo Oscar Nchemwa wakati wa Mafunzo ya usimamizi kwa Wasimamizi na Wasimamizi wasaidizi wapatao 1190 ambao  wamepewa mbinu za kukabiliana na changamoto ambazo zitajitokeza wakati wa zoezi zima la upigaji kura za kuchagua Rais,wabunga na madiwani.

‎Nao baadhi ya Wasimamizi wa vituo vya kupigia kuwa wakazungumzia namna ambavyo watatumia mafunzo hayo vyema na kujiepusha na migongano ya kisiasa au kuwa chanzo cha vurugu.