Thursday , 23rd Oct , 2025

Chama cha wananchi CUF kinaendelea na ziara yake Mkoani Morogoro ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa kampeni zake kuelekea uchaguzi mkuu.

Mgombea urais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya cha cha wananchi CUF Gombo Samandito Gombo amewaasa Watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura ifikapo na kuwapuuza watu wanaoposha na kuhamasisha maandamano.

Gombo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Morogoro ambapo amesema kwamba wananchi hawana njia mbadala ya kuweza kumaliza matatizo yao isipokuwa kwemda kupiga kura na kumchagua kiongozi wanayamtaka.

Mgombea Urais Gombo katika mkutano wake na waandishi wa habari amesema anasikitishwa na tabia ya baadhi ya mawakala wanaonunuliwa wakati  wa kusimamia zoezi hilo la uchaguzi jambo ambalo ameliita ni kinyume cha sheria na kanuni za uchaguzi.

Chama cha wananchi CUF kinaendelea na ziara yake Mkoani Morogoro ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa kampeni zake kuelekea uchaguzi mkuu.