
Carragher, ambaye hajawahi kujitosa kusomea kozi ya ukocha, amejikuta anapuuza mbinu na matumiza ya Kocha Arne Slot kwa Salah wakati mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya England wakipigwa 2-1 nyumbani na Manchester United, ikiwa ni kipigo chao cha nne mfululizo katika michuano yote.
"Jürgen Klopp alikuwa akimuanzisha sana, miaka ya nyuma Mo Salah anaweza kuwa na mchezo mbaya na kutolewa nje hata kama angekuwa na nguvu na nia ya kuendelea na mchezo. Tuko katika hatua ambayo Mo Salah hapaswi kucheza kila mchezo, isiwe kesi ya yeye kila siku lazima awepo kikosi cha kwanza''- Carragher