Thursday , 11th Sep , 2025

Nchini Marekani, mwanaharakati maarufu wa kisiasa na mshirika wa rais Donald Trump, Charlie Kirk, ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa katika chuo kikuu cha Utah.

Rais wa Marekani amelaani kifo cha Charlie Kirk Kirk aliyekuwa alikuwa mmoja wa wanaharakati wahafidhina (Conservative) mashuhuri na mwanahabari nchini Marekani na mshirika wa kutumainiwa wa Rais Donald Trump.

Ameyataja mauaji ya Charlie Kirk 'wakati wa giza kwa Marekani' huku msako mkali ukiendelea kuwapata wahusika wa shambulio hilo, lililowashutua Wamarekani.

Charlie Kirk , 31, aliuawa kwa kupigwa risasi alipokuwa akizungumza katika hafla katika Chuo Kikuu cha Utah Valley.
Hakuna mtu mwingine aliyepigwa risasi wakati wa tukio hilo. 

Mke na watoto wa Kirk walikuwepo wakati wa ufyatuaji risasi, kulingana na Seneta wa Oklahoma Markwayne Mullins
Bado hakuna sababu inayojulikana ya upigaji risasi huo

Mnamo 2012, akiwa na umri wa miaka 18, alianzisha shirika la Turning Point USA, shirika la wanafunzi ambalo linalenga kueneza maadili ya kihafidhina katika vyuo vya Marekani.

Mitandao yake ya kijamii na podikasti ya kila siku iliyojulikana mara nyingi alikuwa akijadiliana na wanafunzi kuhusu masuala kama vile utambulisho wa watu waliobadili jinsia, mabadiliko ya hali ya hewa, imani na maadili ya familia.
Kirk alikuwa ameoa na alikuwa na watoto wawili wadogo, ambao walikuwa naye wakati wa tukio la ufyatuaji risasi.