
Katika taarifa ya Jumapili, vuguvugu la M23 limesema mazungumzo ya amani hayatarejea baina yake na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mpaka masharti yote ya tamko la kanuni yatatekelezwa kikamilifu. Hii ni pamoja na kuachiliwa kwa wafungwa.
Hili linazua hofu kwamba huenda pande hizo mbili zikabadilisha hatua iliyofikiwa kumaliza uhasama ikikumbukwa kuwa mapigano mashariki mwa DRC yaliongezeka mwezi Januari, wakati waasi hao wanaoungwa mkono na Rwanda walipoteka sehemu kubwa ya eneo hilo, ukiwemo mji mkuu wa eneo la Goma.
M23 walitia saini azimio la makubaliano Julai 19, 2025 ambapo waliapa kuanza mashauriano kabla ya Agosti 8 na kwa lengo la kufikia Agosti 18 chini ya juhudi za upatanishi zilizooongozwa na Qatar pamoja na DRC.
Kwa makubaliano haya, pande hizo mbili ziliazimia kusitisha mapigano. Ilitakiwa pia kuandaa njia ya mazungumzo zaidi ya amani, kwa lengo la kufikia makubaliano ifikapo tarehe 18 Agosti.
Jeshi la Kongo wiki iliyopita lilishutumu M23 kwa kutishia kusitisha mapigano kwa kufanya mashambulizi mengi mashariki mwa nchi hiyo. Wakati huo huo M23 wamesema vikosi vya serikali vimeendelea kushambulia maeneo ya waasi hao.