Monday , 21st Jul , 2025

Katibu wa CCM Mkoa wa Mara Iddy Mkowa amekanusha uvumi wa kuibiwa kwa sanduku la kura katika uchaguzi wa Madiwani Viti Maluum Wilaya ya Serengeti.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mara Iddy Mkowa amekanusha uvumi wa kuibiwa kwa sanduku la kura katika uchaguzi wa Madiwani Viti Maluum Wilaya ya Serengeti.

Mkowa aneelezea kuwa kulikuwepo na jaribio la kuporwa kwa sanduku hilo la kura na kijana aliyevalia mavazi ya chama cha mapinduzi ambaye aliingia ndani ya chumba cha kupigia kura na kubeba sanduku moja lakini hakufanikiwa kutokanalo nje kutokana na kudhibitiwa na askari waliokuwepo eneo hilo.

Aidha Mkowa akatoa rai kwa wajumbe pamoja na wagombea kuharibu uchaguzi  kwani kila mmoja atavuna alichopanda.

Vilevile amewaasa wajumbe wasiadaike kwa Kupokea Rushwa kutoka kwa  wagombea kwani watakuwa wanamnunua kiongozi badala ya kupata Kiongozi bora kwani kiongozi anaenunua Uongozi hawezi kuleta maendeleo