Tuesday , 15th Jul , 2025

Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufani (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk leo Julai 15, 2025 amefungua mafunzo ya watendaji wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 Mjini Unguja, Zanzibar ambapo amewasisitiza watendaji hao kuhakikisha vifaa vya uchaguzi wanavyopokea kutoka

Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufani (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk leo Julai 15, 2025 amefungua mafunzo ya watendaji wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 Mjini Unguja, Zanzibar ambapo amewasisitiza watendaji hao kuhakikisha vifaa vya uchaguzi wanavyopokea kutoka Tume, wanavihakiki, kuvikagua na kuhakikisha vinasambazwa kwenye vituo vyote na kila mkuu wa kituo anapata vifaa vyote vya uchaguzi vinavyohitajika mapema.

 

“Wakati wa kuapisha mawakala, toeni taarifa mapema kwa vyama vya siasa kwa mujibu wa sheria, kanuni na maelekezo ya Tume na kuvipatia vyama vya siasa orodha ya vituo vya kupigia kura ili kuviwezesha kupanga mawakala,” amesema Jaji Mbarouk.

 

Jaji Mbarouk amewataka kuhakikisha kuwa siku ya uchaguzi wanaweka utaratibu utakaowezesha kila kituo cha kupigia kura kufunguliwa saa 1:00 kamili asubuhi na kufanya mawasiliano na Tume pale ambapo ushauri utahitajika kuhusiana na masuala ya uchaguzi.