Wednesday , 2nd Jul , 2025

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin wamezungumza kwa simu kwa mara ya kwanza katika karibu miaka mitatu. 

Rais wa Ufaransa na mwenzake wa Urusi wamejadili kuhusu vita vya Ukraine na suala la nyuklia la Iran. 
Hii ni mara ya kwanza tangu Septemba 2022: mazungumzo kati ya Emmanuel Macron na Vladimir Putin.

 
Ikulu ya Élysée imesema kwamba viongozi hao wawili walizungumza kwa "zaidi ya saa mbili kwenye simu." Na katika hali ya kushangaza, vita vya Ukraine, ambavyo vimekuwa vikiendelea tangu jeshi la Urusi lilipoishambulia Ukraine mnamo mwezi Februari 2022, vilijadiliwa.

Kwa mujibu wa Ikulu ya Élysée, rais wa Ufaransa "amesisitiza uungaji mkono usiyotetereka wa Ufaransa kwa uhuru na uadilifu wa eneo la Ukraine" na "akatoa wito wa kuanzishwa, haraka iwezekanavyo, usitishwaji wa mapigano na kuanzishwa kwa mazungumzo kati ya Ukraine na Urusi kwa ajili ya suluhu thabiti na la kudumu la mzozo huo."

Kulingana na ofisi ya rais wa Urusi, Vladimir Putin alimwambia Emmanuel Macron kwamba makubaliano yoyote ya amani nchini Ukraine lazima "yawe ya kina na ya muda mrefu, yatoe uondoaji wa sababu kuu za mgogoro wa Ukraine na kuzingatia ukweli mpya wa eneo"