Monday , 30th Jun , 2025

Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, Dkt. Damas Ndumbaro, leo tarehee 30/6/2025 ameongozana na mke wake kufika katika Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Manispaa ya Songea kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya ubunge kwa kipindi kingine kupitia tiketi ya

Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, Dkt. Damas Ndumbaro, leo tarehee 30/6/2025 ameongozana na mke wake kufika katika Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Manispaa ya Songea kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya ubunge kwa kipindi kingine kupitia tiketi ya chama hicho.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Dkt. Ndumbaro alisema kuwa katika kipindi chake cha uongozi amefanikisha mambo mengi kwa maendeleo ya wananchi wa Songea Mjini. Aliongeza kuwa lengo lake kuu kwa kipindi kijacho ni kuhakikisha Manispaa ya Songea inapandishwa hadhi na kuwa Jiji, hatua ambayo alisema itafungua milango zaidi ya fursa za kiuchumi na kijamii kwa wakazi wa eneo hilo.