Saturday , 28th Jun , 2025

Watu 36 wamefariki dunia na wengine 30 kujeruhiwa baada ya kutokea ajali mbaya leo jioni wilayani Same, mkoani Kilimanjaro.

Mkuu wa Wilaya ya Same,  Kasilda Mgeni, amethibitisha ajali na idadi hiyo ya vifo na Majeruhi

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, yupo eneo la tukio na anatarajiwa kutoa taarifa rasmi muda wowote kuhusu hatua zinazochukuliwa na hali ya waathirika.

Ajali hiyo imetokea katika eneo la Sabasaba, kata ya Same, na imehusisha basi la kampuni ya Channel One lenye namba za usajili T 179 CWL lililokuwa likitoka Moshi kuelekea Tanga kugongana uso kwa uso na basi dogo aina ya Coaster lenye namba za usajili T 199 EFX lililokuwa likitoka wilayani Same, na magari yote mawili yamewaka moto.