
Inaelezwa kuwa Uganda imewasiliana na majirani wa nchi za Mashariki ya Kati kwa msaada wa kuwahamisha raia wake
Kwa kuwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki haina balozi nchini Israeli na Iran, ambazo anga zake zote zimefungwa, inaratibu uokoaji kupitia Misri, Uturuki, Azabaijan na Jordan na imezitaka nchi hizo nne kuwapa raia wake viza.
Wizara ya mambo ya nje iliomba wajumbe wa kidiplomasia nchini Iran na Israeli kuwezesha mchakato huo, huku wanafunzi 48 wakiwa tayari njiani kuondoka Tehran.
Nigeria imesema maandalizi ya kuwarudisha raia wake nyumbani yako karibu kukamilika na kuwashauri kuwasiliana na ubalozi au ujumbe wa karibu wa Nigeria. Nchi hiyo ya Afrika Magharibi ilisema inashirikiana na washirika wa kimataifa ili kuharakisha shughuli hiyo.
Kenya imewataka raia wake kuwa waangalifu sana, kuepuka harakati zisizo za lazima, kukaa ndani inapowezekana na kufuata maagizo ya mamlaka za mitaa
Afrika Kusini hapo awali iliwataka raia wake nchini Iran kujiandikisha kwa ubalozi kwa usalama wao.
Mzozo huo tayari umegharimu maisha ya watu wasiopungua 148.