Tuesday , 27th May , 2025

Tovuti ya takwimu za mpira wa Miguu Duniani (OPTA ANALYST) imeipatia Chelsea asilimia 51.1% za kushinda taji la UEFA Conference League ndani ya dakika 90 dhidi ya Real Betis hapo kesho Jumatano Uwanja wa Tarczyński, nchini Poland majira ya Saa nne kamili usiku.

Chelsea inaweza kuwa timu ya kwanza kuwahi kushinda mataji ya michuano minne mikubwa ya UEFA, baada ya kushinda Kombe la Washindi la UEFA, Ligi ya Mabingwa na Ligi ya Europa.

 

Timu za Uhispania zimeshinda kila fainali kati ya tisa za mwisho za Uropa dhidi ya timu kutoka Uingereza. Timu ya mwisho ya Ligi Kuu ya Uingereza kushinda dhidi ya timu ya La Liga ilikuwa Liverpool dhidi ya Alavés kwenye Kombe la UEFA la 2001 (kwa mikwaju ya penati 5-4).

 

Kikosi cha The Blues chini ya Kocha Enzo Maresca kimefika hatua ya fainali katika michuano hii kwa kuwatoa FC Copenhagen (ilishinda 3-1 kwa jumla ya mabao 3-1), Legia Warsaw (4-2) na Djurgården (5-1). Chelsea wataweka rekodi katika historia, baada ya kushinda Kombe la Washindi la UEFA (1971, 1998), Ligi ya Mabingwa ya UEFA (2012, 2021) na UEFA Europa League (2013, 2019), wakifanikiwa dhidi ya Real Betis watakuwa timu ya kwanza katika historia kushinda mashindano makubwa manne tofauti ya UEFA.