
Mmoja wa wafugaji kutoka maeneo ya katikati mwa Nigeria
Gavana wa jimbo la Benue, Ormin Torsar Victor, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba mwishoni mwa wiki iliyoisha, watu 20 waliuawa kwenye kijiji cha Aondona, miongoni mwao wakiwa watoto wadogo.
Msemaji wa polisi wa jimbo hilo, Anene Sewuese Catherine, amethibitisha mauaji mengine kwenye vijiji vingine, wakiwemo maafisa wa polisi waliokuwa wakikabiliana na washambuliaji.
Jamii ya Fulani, kabila linaloishi kwa kutegemea ufugaji, imekuwa ikipambana mara kwa mara na jamii za wakulima, kila upande ukidai umiliki mkubwa wa ardhi ya eneo la katikati mwa Nigeria.