Saturday , 24th May , 2025

Rais wa zamani wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) Joseph Kabila Rais wa sasa wa taifa hilo Felix Tschisekedi kwa kuiingiza nchi katika machafuko na kutoa wito kwa Wakongo kuungana ili kurejesha sheria na utulivu nchini mwao.

Kabila ameshambulia mfumo wa haki wa nchi hiyo baada ya Seneti kupiga kura ya kuondoa kinga yake, na kumfungulia njia ya kushtakiwa kwa madai ya uhaini na uhalifu wa kivita.

Kabila alitoa hotuba ya moja kwa moja kutoka eneo lisilojulikana baada ya kupoteza kinga yake kwa madai ya uhusiano na kundi la M23, amesema kwamba mfumo wa haki ulikuwa chombo cha ukandamizaji kwa udikteta unaojaribu sana kuendelea kuwa mamlakani.

Kabila mwenye umri wa miaka 53, ambaye anakanusha kuwaunga mkono waasi wanaoungwa wa M23 ambao wameiteka miji miwili mikubwa mashariki mwa nchi hiyo iliyokumbwa na mizozo, amekuwa uhamishoni tangu 2023.