
Kizza Besigye, 68, ambaye alifika mahakamani kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi yake ya uhaini siku ya Jumatano, alitekwa nyara na watu wenye silaha katikati mwa mji mkuu wa Kenya mwezi Novemba na kuibuka tena siku chache baadaye katika mahakama ya kijeshi nchini Uganda.
Hapo awali serikali ya Kenya ilikana kuhusika na utekaji nyara wake.
Katika mahojiano ya na wanahabari Jumanne jioni, Katibu wa Masuala ya Kigeni Musalia Mudavadi alikiri kuwa Kenya ilishirikiana na mamlaka ya Uganda katika suala hilo
Akielezea msimamo wake, Mudavadi alisema Uganda ni taifa rafiki na Kizza Besigye hakuwa akitafuta hifadhi na hakusema kama anatafuta hifadhi