Thursday , 15th May , 2025

Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza limemkamata na linaendelea kumhoji Diana Bundala maarufu kama Mfalme Zumaridi (42), mkazi wa mtaa wa Buguku, Buhongwa mkoani Mwanza, kwa tuhuma za kuendesa shughuli za kidini bila usajili pamoja na kufanya mahubiri kwa waumini wake kwa sauti ya juu.

Mfalme Zumaridi

katika eneo hilo ambalo ni makazi ya watu na kusababisha usumbufu kwa majirani.

Aidha Zumaridi anaendelea kuhojiwa juu ya video yake inayosambaa mitandaoni akiwa na kundi la watoto wadogo wa kike na wa kiume akiwaeleza kuwa yeye ndiye Mungu wao ambaye ana uwezo wa kuwatenganisha na kifo.

Jeshi la Polisi Mwanza limesema uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea, na kwamba litashirikiana na taasisi nyingine za serikali.