Wednesday , 14th May , 2025

Nyota wa zamani wa AC Milan Kaká yuko mbioni kujiunga na timu ya taifa ya Brazil kama kocha Msaidizi chini ya kocha mkuu Carlo Ancelotti anayetarajiwa kujiunga na timu hiyo hivi karibuni 

Carlo Ancelotti na Kaka

Kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini Brazil, Ancelotti anamtaka Kaká ili kuongeza nguvu katika benchi lake la ufundi hatua itakayowakutanisha tena wawili hawa waliowahi  kutamba kwa mafanikio makubwa.

Kaká na Ancelotti waliandika historia ya pamoja ya kuchukua UEFA Champions League msimu wa mwaka (2006/07), Ubingwa wa ligi Serie A (2003/04) wakiwa na AC Milan Kachukua UEFA Super Cup (2003, 2007) pamoja na FIFA Club World Cup (2007)Wakati wanafanya kazi pamoja ndani ya klabu ya AC Milan walifanikiwa kuipandisha katika kileleni cha ubora Barani ulaya. 

Kinachosubiriwa kwa hamu ni kwa namna gani wataifikisha timu ya taifa ya Brazil kwenye kilele cha ubora endapo dili hili likifanikiwa.