Tuesday , 6th May , 2025

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imepanga mechi ya mzunguko wa pili ya Ligi Kuu baina ya Yanga na Simba ‘Kariakoo Derby’ kuchezwa Jumapili Juni 15, 2025.Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imepanga mechi ya mzunguko wa pili ya Ligi Kuu baina ya Yanga na Simba ‘Kariakoo Derby’ kuchezwa Jumapil

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imepanga mechi ya mzunguko wa pili ya Ligi Kuu baina ya Yanga na Simba ‘Kariakoo Derby’ kuchezwa Jumapili Juni 15, 2025.

Ratiba hiyo imeanikwa saa kadhaa baada ya uongozi wa Yanga kutangaza kutokuwa tayari kucheza mchezo huo ambao awali ulikuwa ufanyike Machi 8 mwaka huu.

Mechi ya Machi 8 haikuchezwa baada ya kuahirishwa na TPLB kufuatia vurugu zilizojitokeza katika Uwanja wa Benjamin Mkapa siku moja kabla ya mchezo baada ya Simba kuzuiwa na waliotambulika kuwa ni walinzi wa Yanga ‘makomandoo’ kufanya mazoezi uwanjani hapo.

Ratiba mpya iliyotolewa na TPLB imeonyesha kuwa mechi hiyo ya watani wa jadi itachezwa Juni 15, saa 11:00 jioni.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, mechi za mwisho za Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu zitachezwa Jumapili, Juni 22 mwaka huu.