Monday , 5th May , 2025

Kocha wa Manchester United Ruben Amorim amesema klabu hiyo haipo tayari kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya ‘UCL’

Kocha wa Manchester United Ruben Amorim

United inashika nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi kuu ya England wamepoteza jumla ya michezo 16 ndani ya msimu huu ikiwa ni kiwango kibaya zaidi kwa miamba hiyo ya Manchester kwa kipindi cha miaka 35

Mashetani wekundu watacheza UCL msimu ujao kama watashinda taji la Europa League huku kocha wa klabu hiyo akisema wapo njia panda kuelekea katika msimu mpya wa mashindano 2025-2026

“Bado hatujawa tayari kucheza katika ligi ya EPL na wakati huohuo tushindane katika UCL, na tunalifahamu hilo lakini tunahitaji kushinda michuano hii ili tuwapatie furaha mashabiki wetu na kufuzu ligi ya mabingwa kisha tutakuwa na muda wa kujiandaa na kuendana na kasi ya michuano hiyo yote “ Amesema Amorim wakati akizungumzia mchezo wao wa nusu fainali ya EuropaLeague dhidi ya Athletic Club