Sunday , 27th Apr , 2025

Rais Samia Suluhu Hassan, amepokea ujumbe wa hayati Papa Francis kwa ajili ya Tanzania aliouandika siku chache kabla ya kifo chake akimtakia Rais Samia pamoja na Watanzania kwa ujumla kheri ya maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyoadhimishwa Aprili 26,2025.

Rais Samia Suluhu Hassan

Kupitia ukurasa wake wa X Rais Samia ameambatanisha barua hiyo yenye ujumbe wa Papa Francis ambao alikabidhiwa Balozi wa Vatican hapa nchini.

"Kwa unyenyekevu na shukrani, nimepokea ujumbe wa hayati Papa Francisko kwangu, kwa nchi yetu na kwa Watanzania wote, aliouandika siku chache kabla Mwenyezi Mungu hajamwita kwake, na kumkabidhi Balozi wa Vatican hapa nchini, Askofu Mkuu Angelo Accattino. Tuendelee kumwombea kwa Mwenyezi Mungu alale mahali pema," ameandika Rais Samia