
Kiongozi wa Chama cha People's Liberation Part (PLP), kutoka nchini Kenya, Wakili Martha Karua
Katika mazungumzo yake Wakili Karua amewataka viongozi wa Afrika Mashariki walioko madarakani kuhakikisha wanatenda haki kwa vyama vya upinzani kwa kile alichokitaja kuwa kila raia ana haki kwa nchi yake husika.
"Katiba za nchi zote za Afrika Mashariki zinafanana katika kipengele cha kuwa wanaotoa madaraka ni wananchi na ni wananchi hao ndio wenye uwezo wa kutwaa madaraka hivyo tusinyanyasane," amesema Wakili Martha Karua.
Katika hatua nyingine, awakili huyo na Waziri wa zamani wa Sheria na Haki nchini Kenya, ameshangazwa na kitendo cha Tundu Lissu kutofikishwa mahakamani.