
1. Epuka kuchaji simu yako wakati unacheza gemu au kwenye eneo karibu na jua kali
2. Japo haina madhara ila jitahidi kuondoa simu kwenye chaji ikifika asilimia 100
3. Usiruhusu simu yako ikaisha chaji kabisa, weka chaji ikifika asilimia 20 na unaweza ukaitoa kwenye chaji kama imefika asilimia 80
4. Jitahidi kuondoa kava la simu wakati wa kuweka chaji simu yako ili kuifanya simu ipume na kuzuia ongezeko la joto
5. Kama unapenda kulaza simu kwenye chaji basi jitahidi uruhusu ''Optimized battery charging'' kuipata nenda Settings > Battery > Charging.
6. Epuka kuchaji simu mara kwa mara na hakikisha unatumia chaji sahihi, siyo kila chaji inafaa.
Chanzo: apple.com