Sunday , 23rd Mar , 2025

Shambulizi la anga la Israel katika mji wa kusini wa Khan Younis huko Gaza limemuua kiongozi mkuu wa chama cha Hamas Salah al-Bardaweel.

kiongozi mkuu wa chama cha Hamas Salah al-Bardaweel aliyeuawa

Wenyeji wanasema shambulizi hilo la anga liliua wote wawili Bardaweel, mwanachama wa ofisi ya kisiasa ya kundi hilo pamoja na mkewe.

Jeshi la Israel lilianza tena mashambulizi makubwa dhidi ya Gaza siku ya Jumanne, likiilaumu Hamas, na kuacha makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyoanza tarehe 19 Januari na kuhitimisha takriban miezi miwili ya utulivu.

Hata hovyo Israel haijatoa taarifa yoyote kuhusu shambulio hilo.