
Mzee Mussa Rashid, mkazi wa Tabora
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, ambapo inadaiwa kuwa mzee huyo aliwasili Sumbawanga majira ya saa 4:00 usiku na kukutana na mwenyeji wake, ambaye alimtaka aoge dawa maalum kabla ya tiba kuendelea.
Baada ya muda mfupi, alipelekwa makaburini ambapo alilazwa juu ya kaburi na kuanza kuogeshwa dawa. Ghafla, alitambua kuwa haoni nguo zake, saa yake ya thamani, pamoja na fedha kiasi cha shilingi laki mbili na alitelekezwa hapo akiwa utupu hadi wasamaria wema walipomuokota na kumstiri kwa kipande cha kanga.
Akithibitisha tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Nyakia Ally Chirukile, amewataka Watanzania kuachana na imani potofu za kutafuta utajiri kwa njia za kishirikina. Huku akihimiza wananchi kufanya kazi kwa bidii na kumtanguliza Mwenyezi Mungu badala ya kutegemea waganga wa kienyeji wasiokuwa na uaminifu.