Tuesday , 4th Mar , 2025

Nahodha wa zamani wa Real Madrid Sergio Ramos amefunga bao lake la  kwanza katika klabu yake ya  Monterrey wakati timu hiyo ya Mexico ikiilaza Santos Laguna 4-2 kwenye Uwanja wa Estadio BBVA.

Sergio Ramos - Nahodha wa zamani wa Real Madrid

Ramos  mwenye umri wa miaka 38 alijiunga na  Liga MX mwezi Februari baada ya kuondoka  Sevilla mwishoni mwa msimu wa 2023-24.

Mshindi huyo wa Kombe la Dunia akiwa na Uhispania mwaka 2010, aliunganisha kwa kichwa mpira wa kona na kuifanya timu yake kushinda kwa mabao 2-1, likiwa bao lake la 120 katika maisha ya klabu , akiwa ameifungia Real Madrid mabao 101, 6 akiwa na PSG na 7 akiwa na Sevilla.