Sunday , 2nd Mar , 2025

Kocha wa PSG, Luis Enrique atoa onyo kwa Liverpool kabla ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. PSG watawakaribisha Liverpool siku ya Jumatano Mchi 05/2025.

Luis Enrique - Kocha wa PSG

Mabingwa hao wa Ufaransa wameshinda mechi kumi mfululizo. Enrique ameionya Liverpool na akiutaja mchezo huo kuwa utakuwa "50-50".

"Inaonyesha kiwango chetu cha sasa, tunapaswa kufikiria kuhusu Ligi ya Mabingwa, mechi mbili dhidi ya Liverpool, tufikirie kuwa na njaa ya kushinda"

"Hatutabadilika sana ila itakuwa tofauti, itakuwa ngumu sana, bila shaka, lakini tuko katika kipindi bora zaidi cha msimu. Tutacheza dhidi ya timu bora zaidi ya Ulaya, iliyofuzu kwa ustadi, lakini haipo katika mawazo yetu kubahatisha, kukaa kwa kujilinda, tutashambulia na tutajaribu kufanya hivo"-Kocha  Enrique wa PSG