Tuesday , 25th Feb , 2025

Kila mmoja kwa sasa anafahamu kwamba Dunia inaelekea kwenye ulimwengu wa akili unde

 

Lakini changamoto kwa sasa ni kwa watu kuingia kwenye ulimwengu huu, imekuwa ni changamoto kwa baadhi ya watu kupata taarifa muhimu na za uhakika pale mtu anapotamani kujifunza, hata gharama za baadhi ya programu kwenye ulimwengu wa akili unde zimekuwa za juu.

Ni furaha yetu kukukaribisha kwenye wavuti ambayo itakusaidia wewe kujifunza chochote kwenye ulimwengu wa akili unde ikiwa ndiyo unaanza kujifunza, una elimu kiasi au ni mkongwe kabisa basi wavuti hii itakusaidia sana, wavuti hiyo inaitwa Deeplearning.AI

Hii ni wavuti ambayo itakuwezesha kujifunza kuhusu Akili unde kwenye namna rahisi zaidi, kiasi cha wewe kufahamu hata kutengeneza Application ya kwako mwenyewe.