Monday , 24th Feb , 2025

Bondia Abedi Zugo amepigwa kwa TKO katika pambano liliofanyika usiku wa jana kuamkia  katika raundi ya tatu kutoka kwa bondia Bekman Soilybaev wa Kazakhstan kwenye pambano la raundi  12 na kushindwa kuendelea kupigana.

Bondia Abedi Zugo

Kufuatia ushindi huo kumemfanya bondia Soilybaev kuwa bingwa wa Dunia wa mkanda wa UBO  katika pambano hilo lililofanyika  nchini Kazakhstan katika ukumbi wa Halyk Arena sport complex.

Soilybaev ni bondia  namba 27 Duniani kati ya mabondia 1957 kwa uzani wa Super feather akiwa amecheza mapambano 21 akishinda 20 huku 11 kati ya hayo yakiwa kwa 'KO' na akipoteza pambano moja pekee kwa 'points'.

Kwa upande wake Zugo ni bondia  namba 67 Duniani kati ya mabondia 1957 akiwa amecheza mapambano 16 akishinda 15 na 13 kati ya hayo akishinda kwa 'KO' na kupoteza moja.