Thursday , 20th Feb , 2025

Nyota wa Real Madrid Kylian Mbappe amefikisha mchango wa mabao 500 katika maisha yake ya soka baada ya kupiga hat trick (Magoli matatu) katika mchezo wa jana UCL Real Madrid walipoipiga Manchester City bao 3-1 katika mchezo wa marudiano wa mtoano

Kylian Mbappe - Mshabuliaji wa Klabu ya Real Madrid

Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 26 mpaka sasa amefunga magoli 360 na assist 142 katika ngazi ya klabu na timu ya Taifa

Aidha, Mbappe anakuwa mchezaji wa 6 kufunga hat trick dhidi ya timu inayofundishwa na Pep Guardiola

Wakwanza kufanya hivyo alikuwa Sergio Aguero 2014, Lionel Messi 2016,  Jamie Vardy alifanya mara mbili 2016 na 2020, Christopher Nkunku 2021, Viktor Gyokeres 2024 na Mbappe amefanya hivyo jana 2025

Mbappe amefanya hiivyo jana kwenye ushindi wa 3-1 walioupata Madrid dhidi ya Man City.