Thursday , 13th Feb , 2025

Imeelezwa kuwa uwepo kwa matumizi ya dawa kinga iitwayo PrEP, kumechangia matumizi madogo ya kondomu katika tendo la kujamiiana.

Kondomu

Hayo yamesemwa na Haika Mtui ambaye ni mwakilishi wa Aids Health Care Foundation (AHF), wakati akiwasilisha taarifa ya matumizi ya kondomu ikiwa ni Siku ya Kondomu Kimataifa.

"Hii ni moja ya changamoto ambayo ipo katika mapambano ya kukabiliana na matumizi ya kujikinga na UKIMWI," amesema

Haika amesema siku ya Kondomu ni muhimu ya kutoa elimu ya kupambana na maambukizi ya VVU/UKIMWI.