Wednesday , 12th Feb , 2025

Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Marriane Young ameweka wazi kuwa Uingereza itaendelea kushiriki katika Progaram mbalimbali za kimaendeleo na misaada nchini Tanzania na barani Africa huku akisema wanafuatilia kinachofanywa na Marekani kwa baadhi ya nchi Africa

Balozi Marriane ameyasema hayo alipotembelea vyombo vya habari vya IPP kujionea jinsi vinavyowahudumia watanzania ambapo mbali na kuvipongeza vyombo hivyo amesema kuwa Uingereza inathamini kinachofanywa na Marekani kupitia upya baadhi ya Program zake na wanasubiri matokeo yake huku akisema wao wanaendelea kushiriki katika Program mbalimbali za kimaendeleo Tanzania na nje ya Tanzania

"Ni habari kubwa sana hii kila mtu anafuatilia hilo, tunathamanini kinachofanywa na Marekani kufanya mapitio ya Program zao za misaada na sisi na wengine tunasubiri kuona matokeo yake, ila hilo halituzuii sisi tunaendelea kushiriki kikamilifu katika Program mbalimbali za kimaendeleo kimataifa na mifumo yetu ya kibinaadamu"

Akizungumzia uhusiano wa kidiplomasia uliopo baina ya Tanzania na Uingereza amesema nchi hizo zipo kwenye uhusiano wa muda mrefu na wenye nguvu ambao umevuka sasa na kupelekea mashirikiano katika maeneo mbalimbali yakiwemo Biashara, Afya, Elimu, ulinzi na maeneo mengi ya maendeleo 

"Tuna ushirikiano mzuri sana wa kidiplomasia tena wenye nguvu sana ambao umetupeleka mbali na kutusaidia kushirikiana kwenye maeneo muhimu kama biashara, Ulinzi, na maendeeleo ya afya na elimu pamoja na maeneo mengine ya maendeleo"

Akizungumzia uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika mwaka huu wa 2025 balozi huyo amesema wanasubiri kwa hamu kushughudia uchaguzi huo na ni nafasi kwa umma kuchagua nani aongoze taifa kwa wakati huu huku akisema anaamini mchakato utakuwa wa huru na haki 

"Wote tunavutiwa kufuatilia uchaguzi huo, nin kipindi kinachovutia kweli na ni nafasi kwa watu kuchagua watu wanaowataka wawaongoze katika kipindi husika, tunaamini utakuwa mchakato wa huru na haki ambao pia utazalisha Rais ambaye pia ataendeleza zile 4Rs"

Balozi Marriane Young akiambatana na maafisa wengine wa Ubalozi wa Uingereza Tanzania ametembelea vyombo vya habari vya IPP. ikiwemo East AfricaTV, East africaRadio, Radio One, ITV, Capital Radio na TV, pamoja na Magazeti ya Nipashe na The Guardian