Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini (NECTA) Dkt. Said Mohammed
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini (NECTA) Dkt. Said Mohammed amesema ufaulu wa kidato cha nne umeongezeka kwa mwaka 2024 ukilinganisha na mwaka 2023.
Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar Es Salaam wakati akitangaza matokeo ya kidato cha nne Dkt. Mohammed amesema “takwimu zinaonyesha kuwa ufaulu wa jumla umepanda kwa asilimia 3% kufikia 92.37% ambapo jumla ya watahiniwa 477, 262 kati ya 516, 695 wenye matokeo wamefaulu kwa daraja la kwanza mpaka la nne (Div I -IV)”
Dkt. Mohammed amesema ufaulu huo umepanda ukilinganishwa na wa mwaka jana wa 2023 ambapo watahiniwa waliofaulu walikuwa 471,427 sawa na asilimia 89.36%
Dkt. Mohammed ameongeza kuwa ufaulu kwa watahiniwa walipata daraja kwanza mpaka la tatu Div I-III umeongezeka kwa asilimia 5.54% ukilinganisha na mwaka 2023.
“Watahiniwa wa Shule waliopata ubora wa ufaulu katika Madaraja ya I- III ni 221,953 sawa na asilimia 42.96%. Mwaka 2023 watahiniwa waliopata ufaulu wa Madaraja ya I-III walikuwa 197,426 sawa na asilimia 37.42%. Hivyo, ubora wa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 5.54 ikilinganishwa na mwaka 2023.” amesema Dkt. Mohammed