Thursday , 9th Jan , 2025

Manula ametemwa na Simba kwenye kikosi cha wachezaji 22 waliosafiri kuelekea Nchini Angola kwenye mchezo wa 5 wa hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bravos Do Maquis utakaopigwa Januari/12/2025.

Zikiwa zimesalia siku 6 pekee dirisha dogo la usajili Tanzania bara kufungwa Januari 15/2025 ambalo lilifunguliwa Disemba 15/2024, Jina la Aishi Salum Manula mwenye umri wa miaka 29 ni miongoni mwa wachezaji wa Simba Sc ambao hawajapata nafasi ya kucheza chini ya Kocha wa Fadlu Davids kwenye mechi za ushindani msimu huu kutokana na kiwango bora anachoonesha Moussa Camara raia wa Guinea.

Golikipa huyo namba 1 wa timu ya taifa ya Tanzania amekuwa kwenye mgogoro na Waajiri wake Simba SC kutokana na sababu za kushuka kwake kiwango baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu alipokuwa akiuguza majeraha yake.

Wakati wa dirisha kubwa la usajili Manula aliweka wazi kutaka kuondoka klabu hiyo ili aende sehemu ambayo atapata muda wa kucheza ili kukiimairisha kiwango chake kuelekea mashindano ya CHAN yanayotarajiwa kufanyika nchi za Tanzania,Kenya na Uganda lakini ilishindikana kuhama.

Kusajili kwa Moussa Camara kwenye kikosi cha Wekundu wa Msimbazi umezidi kuifanya nafasi ya Manula kuwa finyu zaidi na kuna tetesi anaweza kutimkia kwenye moja ya timu zinazoshiriki ligi kuu Tanzania bara.Kwa manufaa mapana ya taifa Golikipa huyo aliyeshinda tuzo ya Golikipa bora wa mwaka mara 5 mfululizo anapaswa kuhama ili taifa liwe kwenye mikono salama kuelekea mashindano ya CHAN 2025 yatakayoanza Februari 1 na kutamatika Februari 28.