Thursday , 26th Dec , 2024

Magonjwa yasiyo ambukiza kama kisukari, saratani na figo yameelezwa kuchangiwa kwa unene na uzito kupita kiasi kwa mrundikano wa mafuta ya ziada au yasiyo ya kawaida mwilini yamekuwa yakichangia kudhoofisha mwili.

Afisa lishe kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala Bw. Walbert Mgeni akifafanua kuhusu makundi mbalimbali ya vyakula na namna yanavyotakiwa kutumiaka.

Magonjwa yasiyo ambukiza kama kisukari, saratani na figo yameelezwa kuchangiwa kwa unene na uzito kupita kiasi kwa mrundikano wa mafuta ya ziada au yasiyo ya kawaida mwilini yamekuwa yakichangia kudhoofisha mwili.

Madhara yatokanayo na unene uliopita kiasi kama kupata magonjwa yasiyo ambukiza yamebainishwa na Afisa lishe kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala Bw. Walbert Mgeni akifafanua kuhusu makundi mbalimbali ya vyakula na namna yanavyotakiwa kutumiaka.

"Mpangilio usio sahihi katika kutumia makundi hayo ya vyakula unaweza kuleta athari katika ubora wa afya ya lishe ikiwemo kusababisha unene uliopitiliza ambao utahamasisha magonjwa yasiyo ambukiza".Amesema Bw. Walbert Mgeni, Afisa Lishe Hospitali ya Rufaa Mkoa Mwananyamala Dar es Salaam.

Baadhi ya vijana Jijini Dar es Salaam wameeleza kuwa unene uliozidi kupita kiasi umekuwa ukisababishwa na mtindo wa maisha wa kutofanya mazoezi na kula vyakula ambavyo vinamafuta mengi.

"Watu wengi wamekuwa wakitumia vyakula vya mafuta kwa wingi kama chips au nyama sana ambavyo vinakwenda kuongeza unene kwenye mwili na kuleta madhara". Amesema Danford Isack Mkumbo, Mkazi wa Singida.

"Watu hawachagui vyakula na hawapangilii mlo vizuri una kuta mtu anakula baga pizza, nyama , nyamachoma, mishkaki kila siku badala yakubadili hata mbogamboga". Amesema Abubakar Hillary Ndembo, Mkazi wa Kivule Dar es Salaam.

Katika kupambana na magonjwa yasiyo ambukiza yatokanayo na unene ulio zidi wameshauri kuweza kufanya mazoezi ambayo yatasaidia kupambana na hali ya unene uliokithiri.

"Hii inatkuta sana tunaopenda kula chips au kiepe hiyo inatupelekea sana kupata obesity kutokana na kula vile vitu vya mafuta na kuwa na miili mikubwa hususani tunapata vitambi na pia tunakuwa na ukosefu wakufanya kazi vizuri". Amesema Vivian Kanza, Mkazi wa Mbezi Beach Dar es Salaam.

"Mazoezi yanajenga mwili kutokuwa na unene pia inabidi kwenda kupata ishauri kwa madaktari virutubisho sahihi kutokana na mwili wako". Amesema Frank Shayo, Mkazi wa Mabibo Dar es Salaam.

"Watu ambao unakuta ni wanene wanene unakuta hawajiamini na furaha yao inapungua chakushauri tusiangalie chakula flani kipo kwenye fasheni sijui chipsi kuku". Amesema Lameck Sinda, Mkazi wa Ubungo Dar es Salaam.

Ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa ya 2022 inaonyesha kwamba magonjwa haya yasioambukiza, ambayo kwa kawaida yanaweza kuepukika na yanayosababishwa na maisha yasiozingatia afya bora yanasababisha vifo vya watu milioni 41 kila mwaka, ikiwemo watu milioni 17 walio chini ya miaka 70.