Wednesday , 18th Dec , 2024

Yanga SC itashuka uwanjani kesho kucheza mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya timu ya Mashujaa kutoka Kigoma kesho saa 10:00 jioni uwanja wa KMC Complex Mwenge Dar es salaam.

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Sead Ramovic raia wa Ujerumani imeshinda mchezo mmoja tu dhidi ya Namungo FC ikipoteza dhidi ya Azam FC, Tabora United,Al Hilal,MC Algers na kutoka sare dhidi ya TP Mazembe katika mchezo wa makundi wa ligi ya mabingwa Afrika.

Yanga SC itashuka uwanjani kesho kucheza mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya timu ya Mashujaa kutoka Kigoma kesho saa 10:00 jioni uwanja wa KMC Complex Mwenge Dar es salaam.

Mchezo huo ni muhimu kwa kikosi hiko bingwa mtetezi wa ligi kuu bara kutokana na mwenendo mbovu wa matokeo iliyokuwa ikiyapata kwa siku za karibuni.

Timu hiyo inayonolewa na Kocha Sead Ramovic raia wa Ujerumani imeshinda mchezo mmoja tu dhidi ya Namungo FC ikipoteza dhidi ya Azam FC, Tabora United,Al Hilal,MC Algers na kutoka sare dhidi ya TP Mazembe katika mchezo wa makundi wa ligi ya mabingwa Afrika.

Yanga SC inashika nafasi ya 4 katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara inahitaji kushinda mchezo wa kesho ili kurudisha hali ya kujiamini na kufufua matumaini yake ya kutetea ubingwa wa ligi pamoja na kombe la shirikisho la CRDB.

Wachezaji wengi ya kikosi cha Wananchi hawapo kwenye viwango vyao vya kawaida vilvyozoeleka hivyo kupelekea nzima kutokucheza kwa ubora uliozoeleka.

Kupoteza michezo miwili mfululizo ilipelekea kufukuzwa kazi kwa aliyekuwa Kocha mkuu wa timu hiyo Miguel Gamondi na nafasi yake kuchukuliwa na Mkufunzi wa sasa Ramovic.

Mchezo dhidi ya Mashujaa hautokuwa rahisi kutokana na ubora wa Mwalimu Abdallah Barres aliye na uzoefu mkubwa wa kucheza michezo mikubwa kama wa kesho dhidi ya timu kubwa.

Kupoteza dhidi ya Wazee wa mapigo na mwendo kunaweza kuamsha presha mpya kwa Viongozi wa Yanga SC kutoka kwa Mashabiki wa timu hiyo kuhusiana na ubora wa Kosha Sead Rmovic na malengo ya klabu hiyo kwa msimu huu.