Friday , 13th Dec , 2024

Kuanzia mwezi wa 4 mwakani, wafanyakazi wa serikali kutokea mji mkuu wa Taifa la Japan, Tokyo watakuwa wanufaika wa kwanza wa mfumo wa kupunguziwa siku za kufanya kazi katika wiki, kutoka siku 5 hadi 6 mpaka kufikia siku 4 pekee katika wiki.

 

 

 

Hivyo wafanyakazi wa serikali kwenye jiji la Tokyo watapata siku 3 za mapumziko kwenye kila wiki, Haya yanajiri baada ya nchi ya Japan kuona ipo haja kuwapa nafasi wananchi wake kupata uwiano sawa wa muda wa kazi na muda wa kukaa na familia zao, hoja nyingine ni kuongeza idadi ya watu wanaozaliwa kwa wananchi kutumia muda mwingi na familia zao, na kuondokana na rekodi ya uwepo wa watu wenye umri mkubwa zaidi Duniani kwenye taifa hilo.

 

Kwa sasa kwenye taifa hilo wastani wa umri wa mwanaume kuishi ni miaka 81.09 huku mwanamke ikiwa ni miaka 87.14 na takwimu za mwisho za mwaka 2023 zinaonesha taifa hilo linajumla ya watu Milioni 124.5