Thursday , 12th Dec , 2024

Takribani watu milioni 34.6 hufariki kila mwaka duniani kutokana na magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo saratani, magoniwa ya moyo, shinikizo la damu, kiharusi na magoniwa ya kisukari, huku Watanzanikumbushwa kuzingatia mtindo wa maisha kukabiliana na magonjwa hayo.

Prof.Mohamed Janabi, Mkurugenzi Hospitali ya Taifa Muhimbili na Mshauri wa Rais waswala ya Afya na Tiba

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Mshauri wa Rais kwenye maswala ya Afya na tiba , Profesa Mohamed Janabi leo wakati anaongea na waandishi wa habari Hospitalini hapo.

“magonjwa ya moyo, shinikizo la damu, kiharusi na ugonjwa wa kisukari huua asilimia 364 zaidi ya ugonjwa wa saratani kwa mwaka, hivyo jamii inatakiwa kuweka msukumo wa kukabiliana na magonjwa haya kutokana na madhara yake”, Prof. Mohamed Janabi, Mkurugenzi Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Aidha Profesa Janabi anawakumbusha wananchi namna bora ya kuepukana na magonjwa haya.
"Suluhisho la magoniwa haya ni kubadili mtindo wetu wa maisha kwa kulala sawasawa, kufanya mazoezi, kuongeza mbogamboga, matunda na kupunguza msongo wa mawazo,Na kwa kiasi kikubwa magoniwa haya yanaathiri nchi hizi zinazoendelea"Prof. Mohamed Janabi, Mkurugenzi Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Aidha baadhi ya wananchi wameomba Serikali kuongeza elimu namna bora ya kuepukana na magonjwa hayo.
“Tunaomba Serikali iongeze elimu wazazi tunaumia kuona vijana wadogo wanahangaika na magonjwa haya kwa kutokuwa na uelewa wa madhara ya magonjwa haya”,Annie Kobelo, mkazi wa Dar es Salaam.

“Mimi nashauri wananchi wenzangu tuzingatie sana ulaji wetu kwa maana vitu vidogo vya kuepuka vinaweza kugharimu maisha yetu yote na tusisahau kumtanguliza Mungu”, Fadhil Agustino, Mkazi wa dar es Salaam.

“Ukijua malengo yako ni yapi ina maana utakuwa makini na vihatarishi vyote ambavyo vinaweza kugharimu uhai wao, nashauri tusihisahau sana kwenye mitindo yetu ya maisha ili tuweze kufanikiwa kwenye hili”, Shabani Kassim, Mkazi wa Dar es Salaam.