Monday , 25th Nov , 2024

Watu 9 wa familia moja katika mtaa wa Bugosi mkoani Mara wamesombwa na maji katika mto Mori kufuatia mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha mito na madaraja kujaa maji ambapo miili ya marehemu 7 imepatikana katika kingo za mto huo huku watu wawili wakiwa bado hawajapatikana.

Mto

Kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha wilayani Tarime Mkoani Mara baadhi ya mito imekuwa ikijaa maji na kuwa hatarishi kwa wananchi ambao wanaishi pembezoni mwa mto pamoja na watumiaji wa barabara hususani katika madaraja.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Tarime anatoa wito kwa jamii kuchukua tahadhari hususani katika kipindi hiki cha masika.