Monday , 25th Nov , 2024

Jeshi la polisi mkoa wa Kagera limepokea magari matano kwa ajili ya kuimarisha Usalama mkoani humo katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa

Kamanda wa Police mkoa wa Kagera SACP Brasius Chatanda amesema jeshi hilo limejipanga kuimarisha ulinzi na Usalama wakati wa uchaguzi huo na  kuhakikisha wananchi wanapiga kura kwa amani na utulivu.

SACP Brasius Chatanda amesema kuwa mkoa utaendelea kuwa salama wakati na baada ya uchaguzi na kuwataka wananchi kutokuwa na hofu na kujitokeza kwa wingi kupiga kura.

"Tumejipanga na sasa tumepokea magari matano yatatusaidia kwenye utendajikazi, zoezi la uchaguzi litaenda salama wananchi mjitokeze kupiga kura na niwahakikishie mkoa wa Kagera utakuwa na amani sasa, wakati wa uchaguzi na hata baada ya uchaguzi"