Stars inahitaji matokeo ya ushindi kama inahitaji kufuzu kwa mara ya tatu mfululizo mashindano hayo baada ya kufanya hivyo 2019,2023 inayosubiriwa kuona tutapata matokeo ya ushindi dhidi ya Guinea, Tanzania itakuwa imejihakikishia kufuzu AFCON kwa mara ya nne katika historia yake 1980,2019,2023 na 2025.
Timu ya taifa ya Tanzania taifa Stars kesho itakipiga dhidi ya timu ya Guinea kwenye mchezo wa kuwania kufuzu mashindano ya kombe la mataifa Afrika AFCON 2025 yatakayofanyika nchini Morocco.Stars inatakiwa kushinda mchezo wa kesho ili kukata tiketi ya kucheza mashindano hayo makubwa kwa timu za taifa Afrika.
Mchezo wa kesho utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Stadium unatazamiwa kuwa ni fainali kwa timu zote mbili kutokana na nafasi zilizopo kwenye kundi H ambapo timu ya Congo DRC imeshafuzu ikiwa na alama 12.Guinea inashika nafasi ya pili imejikusanyia alama 9 baada ya kucheza michezo mitano ushindi wa Jumamosi dhidi ya Congo DRC umeifanya timu hiyo kuishusha taifa Stars mpaka nafasi ya tatu.Stars inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 7 baada ya michezo mitano.
Stars inahitaji matokeo ya ushindi kama inahitaji kufuzu kwa mara ya tatu mfululizo mashindano hayo baada ya kufanya hivyo 2019,2023 inayosubiriwa kuona tutapata matokeo ya ushindi dhidi ya Guinea, Tanzania itakuwa imejihakikishia kufuzu AFCON kwa mara ya nne katika historia yake 1980,2019,2023 na 2025.
Guinea inahitaji alama moja tu ili kufuzu hivyo kuufanya mchezo wa kesho kuwa mgumu kutokana na utofauti wa uhitaji wa timu zinazokutana kesho.Stars haijawahi kucheza mchezo wa kufuzu kwenye mazingira magumu namna hii wakati inafuzu 2019 ilicheza dhidi ya Uganda ambayo ilikuwa ishafuzu 2023 mhezo wa mwishi ilicheza dhidi ya Algeria ambayo nayo haikuhitaji kuwa kwenye presha kubwa hivyo Wachezaji watahitaji zaidi ya kujituma ili kuhakikisha Tanzania inafuzu mashindano ya mwakani nchini Morocco.
Kocha Hemed Suleiman alifanya marebisho kwenye kikosi chake kwa kuwaita Wachezaji wenye uzoefu Mbwana Samatta, Aishi Manula na Saimon Msuva ili kuhakikisha timu inafuzu.Huu ni wakati ambao Wachezaji wenye uzoefu kuibeba timu kutokana na kucheza mechi nyingi zenye ushindani na presha kubwa kwa timu ya taifa mpaka vilabu wanavyovitumikia.
Benchi la ufundi linahitaji kuwaandaa Wachezaji kisaikolojia kuwaondolea presha na hofu ya mchezo wa kesho wakiruhusu wachezaji kuingia kiwanjani huku wakiwa na msongo wa mawazo kucheza dhidi ya Guinea kulingana uhitaji wa kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania kupata matokeo chanya kuwa mkubwa wanaweza kupoteza hali zao za kujiamini.
Hii ni nafasi ya Wachezaji kuandika historia yao kwenye mioyo ya Watanzania kama watafanikisha taifa Stars kufuzu kucheza michuano ya AFCON.Ikitokea Stars ikafanikiwa kufuzu watakuwa na sehemu kubwa ya kuimbwa kutokana na kuiwezesha timu kucheza michuano hiyo mikubwa ya timu za taifa mara tatu mfululizo 2019,2023 na 2025.
Mchezo wa taifa Stars dhidi ya Guinea utachezwa kesho uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10:00 za jioni kwa majira ya Afrika ya Mashariki.Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF imetyangaza hakuna viingilio ili kutoa fursa kwa Watanzania kwenda kuishangilia timu yao ya taifa.