Thursday , 14th Nov , 2024

Ripoti kutoka nchni Ujerumani zinaripo kuwa timu za Ligi kuu Uingereza Manchester united na Arsenal zinamuwania winga wa Bayern Munich ya Ligi kuu Ujerumani Leroy Sane. Sane raia wa Ujerumani mkataba wake na Bayern unamalizika mwishoni mwa msimu huu wa 2024-25.

Leroy Sane Winga wa kimataifa wa Ujerumani na klabu ya Bayern Munich.

Bado hakuna mazungumzo ya pande zote mbili kati ya Bayern Munich na mchezaji Sane kuhusu mkataba mpya na kwa mujibu wa taarifa kama winga huyo atakubali kusalia ndani ya kikosi cha The Bavarians, basi atakatwa asilimia 25 ya mshahara wake wa sasa kutoka Pauni million 16.6 hadi million 12.4.

Kwa upande mwingine ushindani wa namba pia ni mkubwa kwenye kikosi cha Bayern Munich Sane mwenye umri wa miaka 28 anawania namba na wachezaji Michael Olise, Serge Gnabry na Kingsley Coman.