Thursday , 7th Nov , 2024

Kikosi cha Yanga Sc kitashuka dimbani leo kucheza mchezo wa kumi Ligi Kuu soka Tanzania bara leo dhidi ya Tabora United Uwanja wa Azam Complex  Chamazi majira ya Saa kumi na mbili za jioni

Takwimu za mechi mbili walizokutana zinaonyesha timu ya Wananchi imeshinda michezo yote miwili dhidi ya Wapinzani wao siku ya leo  (3-0, 1-0)  Tabora United kutokea Tabora ambayo inashika nafasi ya 10 ikiwa imevuna alama 14 msimu huu.

Kikosi cha Yanga Sc kitashuka dimbani leo kucheza mchezo wa kumi Ligi Kuu soka Tanzania bara leo dhidi ya Tabora United Uwanja wa Azam Complex  Chamazi majira ya Saa kumi na mbili za jioni.

Kikosi hiko kinacholewa na Kocha raia wa Argentina Miguel Gamondi kitawakosa wachezaji wake muhimu wa kikosi cha kwanza akiwemo Dickson Job ambaye anatumikia kadi tatu za njano Ibrahim Hamad Bacca anayetumikia adhabu ya kadi nyekundi aliyooneshwa kwenye mchezo dhidi ya Azam Fc ambao walipoteza kwa 1-0.

Kouassi Yao ambaye ni majeruhi ataukosa mchezo huu kama ilivyo baadhi ya michezo iliyopiya ya mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania.Nafasi yake imekuwa ikechezwa na Wachezaji tofauti Denis Nkane, Maxi Nzengeli na Dickson Jobu.Tabora United wataingia katika mchezo huu wakiwa wametoka kushinda michezo miwili mfululizo dhidi ya Pamba pamoja na Mashujaa.

Takwimu za mechi mbili walizokutana zinaonyesha timu ya Wananchi imeshinda michezo yote miwili dhidi ya Wapinzani wao siku ya leo  (3-0, 1-0)  Tabora United kutokea Tabora ambayo inashika  nafasi ya 10 ikiwa imevuna alama 14 msimu huu.

 

Simba Sc inaongoza msimamo wa ligi kuu TPL kwa alama 25, Yanga imeshuka mpaka nafasi ya pili ikiwa na alama 24 kabla ya kucheza mchezo wa leo.

Miguel Gamondi amesikika akizungumzia ratiba ya ligi inavyozibana timu kwa kukosa muda wa kupumzika kwa kucheza mechi nyingi kwa mfululizo ataliongoza Jeshi lake dimbani leo kucheza mchezo wake wa 7 ndani ya siku 21.

Ligi ya msimu huu inaonekana itakuwa ngumu kutokana na matokeo yanayojinyesha mapema baada ya michezo 10 ya ligi inatoa picha ya ushindani uliopo msimu huu wa 2024-2025, kutokana na vikosi vingi kuimarika kwa kuleta Makocha wazuri pamoja na kusajilili vizuri. Tusubiri tuone je Wananchi watafanikiwa kulejea kileleni mwa ligi kuu Tanzania bara kwa ushindi dhdi ya Tabora United leo.