Friday , 1st Nov , 2024

Tangu aingie madarakani Machi 2021 hadi Agosti 2024, Rais Samia Suluhu Hassan ameufungua uchumi wa Tanzania kwa dunia na kujenga mazingira bora ya biashara za kimataifa. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alivyokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Kiongozi Mkuu wa USAID Isobel Coleman

Matokeo ya juhudi hizo yanaonekana katika ukuaji wa biashara kimataifa, kutoka USD 17.4 bilioni (mauzo nje - dola bilioni 8.4, uingizaji bidhaa - dola bilioni 9) hadi kufikia dola za Kimarekani bilioni 31.4 (Mauzo nje - dola bilioni 15, uingizaji bidhaa - dola bilioni 16.4), hii ikiwa ni sawa na ongezeko kubwa la 84%

Wakati ikishudiwa ongezeko hilo la kibiashara, deni la nje limeongezeka kwa asilimia 33%, kutoka dola bilioni 24.4 hadi dola bilioni 32.6, ambalo jambo limetajwa kuwa ni la kawaida kwa nchi zinazopiga hatua za kimaendeleo kupitia uwekezaji wa kimkakati. 

Kwa kufanya hivyo, Rais Samia amefungua milango ya fursa mpya kwa Watanzania na kukuza uchumi kwa kuhakikisha Tanzania inakuwa sehemu ya ushindani wa kibiashara duniani. 

Chanzo Benki Kuu ya Tanzania 'monthly Economic Review May 2021 and Monthly Economic Review for October 2024'