Klabu ya Manchester City usiku wa jana ilitolewa nje ya mashindano ya kombe la Carabao baada ya kupoteza mchezo dhdi ya Tottenham Hotspurs kwa kufungwa goli 2-1, haikua siku nzuri ofisini kwa Vijana wa Pep Guardiola ugenini White Hart Lane.
Klabu ya Manchester City usiku wa jana ilitolewa nje ya mashindano ya kombe la Carabao baada ya kupoteza mchezo dhdi ya Tottenham Hotspurs kwa kufungwa goli 2-1, haikua siku nzuri ofisini kwa Vijana wa Pep Guardiola ugenini White Hart Lane.
Guardiola alipumzisha baadhi ya Wachezaji wake kutokana na hali ya majeruhi yanaikabili timu hiyo kwasasa ambapo Wachezaji wake wengi wapo kwenye vyumba vya matibabu wanauguza majeraha. Kevin De Bruyne, Rodri majina makubwa na muhimu kwenye kikosi cha Mbingwa watetezi wa ligi kuu Uingereza wanakosekana na kupelekea Manchester City kupungua makali yake na mkufunzi wa kikosi hiko kulazimika kufanya mzunguko wa Wachezaji ili kupumzisha nyota watakaomsaidia kwenye michezo ya ligi kuu.
Kikosi cha The Citizens hakikuwa na Erling Haaland,Mateo Kovačić,Jérémy Doku,Bernardo Silva na Joško Gvardiol ugenini dhidi ya Tottenham. Pep Guardiola baada ya mechi alizungumza na Waandishi wa habari na kukiri kwamba timu yake inawachezaji 13 ambao wapo fiti kucheza na ambao huwa wanacheza kwenye kikosi cha kwanza cha timu yake.
Kutolewa kwenye mashindano ya kombe la Carabao kunaweza kukawa ni faraja kwa timu hiyo inayotumia uwanja wa Etihad, itakuwa imepenguza mgandamizo wa michezo kwenye ratiba yake kama ingeendelea kwenye hatua inayofuata ya mashindano hayo inamaanisha kuna michezo mingine ingeongezeka kwao ingepelekea ugumu kwenye kutetea ubingwa wake kutokana na ongezeko la michezo.
Chelsea FC, Aston Villa, Manchester City na Brighton and Holve Albion timu zinazoshiriki ligi kuu Uingereza zimetolewa kwenye michuano hiyo katika hatua ya 4 bora huku Manchester United, Newcastle United, Arsenal na Liverpool zimefanikiwa kuingia kucheza hatua ya robo fainali ya kombe la Carabao.
Pep raia wa Hispania aliweka wazi kabla ya mchezo huo dhidi ya Tottenham angeanzisha kikosi cha pili kutokana na hali ya majeraha kikosini hivyo kumlazimisha kufanya maamuzi magumu ya kupanga kikosi chake kwa kuangalia ratiba za ligi kuu kulingana na ugumu wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu.