Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na watafiti wa Chuo Kikuu cha London umebaini usingizi wa mchana una faida mbalimbali ikiwemo kuweka sawa utendaji kazi wa ubongo na kuchelewa kuzeeka kwa miaka mitatu hadi sita.
Japokuwa wataalamu hao wanapendekeza kulala chini ya nusu saa, pia wamebaini kuwa ubongo wa watu wanaopata muda kidogo wa kualala ulikuwa na sentimita za ujazo wa 15 sawa na inchi 0.9.
Wataalamu hao wameongeza kuwa kwa wale wanaofanya kazi mchana, usingizi wao ni wa nadra sana usiku kutokana na kubanwa na kazi nyingi.
Picha: Kwa msaada wa mtandao.